KITUO cha Polisi Wazo Hill jijni Dar es
Salaam kimeingia lawamani baada ya kudaiwa kuwaachia watuhumiwa wa makosa ya
kugushi nyaraka ili kujimilikisha eneo la ardhi huku wakijua si la kwao.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha
Mabwepande ambapo watuhumiwa hao walifikishwa kwenye Mahakama ya Ardhi wilayani
Kinondoni mwaka 2014 nakubainika kuwa wana kesi ya kujibu.
Mmiliki halali wa eneo hilo, Samuel
Augastino, akizungumza leo, alisema waligushi
nyaraka kisha kuuziana wenyewe kinyume cha sheria.
Aliwataja watu hao kuwa ni Athuman
Mnubi, Joseph Mponda na Jacob Pius, ambaye inadaiwa kuwa ni raia wa Msumbiji.
"Athuman Mnubi akijifanya mmiliki
wa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari moja na nusu aliliuza kwa sh. 60,000 ambapo
mnunuzi alikuwa ni Jacob Pius haya yamefanyika Novemba 25, 1999,"alisema
Augastino.
Alisema baada ya kesi hiyo kendelea
kusikilizwa kwa muda mrefu watuhumiwa waliagizwa na Mahakama kupeleka vielelezo
vinavyoonesha uhalali wa umiliki wao.
Augastino, alisema baada ya kupeleka
vielelezo hivyo, Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo ndipo alipobaini kuwa
nyaraka hizo zilizowasilishwa nakamanain zilikuwa za gushi.
"Hakimu alibaini hayo Agosti 13
mwaka jana jambao ambalo alitufahamisha kwamba vielelezo hivyo vilikuwa vya
kugushi kwa hiyo akatutaka tuchukue hatua,"alisema Augastino.
Alida kutokana na kitendo hicho hakimu aliwashauri
waende polisi kutoa taarifa ili watuhumiwa hao wachukuliwe hatua za kisheria.
Augastino, alisema kweli walifanya
hivyo, Agosti 13 mwaka jana, kikatolewa kibali na polisi cha kukamatwa
(WH/RB/6812/2015), ambapo walikamatwa kisha kufunguliwa kesi ya kugushi
nyaraka.
Hata hivyo, alidai kuwa baada ya
kukamatwa watuhumiwa hao waliachiwa siku iliyofuata bila ya walalamikaji kupewa
maelezo ya kuachiwa kwa watuhumiwa hao.
"Tumejaribu mara kadhaa kumuona
Mkuu wa Kituo cha Wazo lakini ilishindikana kwani kila tulipofika tuliambiwa
hapatikani kitendo ambacho kilitusikitisha na hii imetufanya tukimbilie kwenye
vyombo vya habari ili kilio chetu kiwafikie wakubwa mbali waliko,"alisema
Augastino.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Christopher Fuime, akitolea ufafanuzi malalamiko hayo, aliwashauri walalamikaji
hao waende katika kituo hicho kwa ajili ya kumuona mkuu wa kituo hicho.
Alimtaka mkuu huyo wa kituo
kulishughulikia suala hilo kwa vile liko katika kituo chake na endapo watakosa
msaada basi warudi kwake tena hata hivyo, anaaminini kuwa watasaidiwa.
No comments:
Post a Comment