BAADHI
ya watumiaji wa simu za kiganjani wamepinga uwamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu itazima simu zote bandia zilizoingizwa
nchini.
Hivi
karibuni TCRA imekaririwa na vyombo vya habari ikiwataka watumiaji wa simu za
mkononi kote nchini kuhakikisha simu wanazotumia zinakuwa na
namba ya utambulisho (IMEI NUMBER), kwa lengo la kuzuia
wafanyabishara wasio waaminifu kuendelea kuingiza simu bandia nchini.
Wakizungumza
jijini Dar es Salaam jana, kwa nyakati tofauti, watumiaji hao walisema wanauhakika
mpango huo utakapotekelezwa utaathiri watu wengi wenyekipato cha chini ambao
ndiyo wanunuzi wa simu hizo.
Fahdy
Juma, alisema hawakubaliani na uwaamuzi huo kwa vile wanaamini kuwa makosa
yaliyosababisha wamiliki simu kizo bandia hayawahusu na baadala yake wakuadhibiwa ni
wafanyabiashara waliyoziingiza.
“Angalia
tangu walipotangaza kwamba watazima simu hizo bandia hakuna hatua yeyote
iliyochukuliwa na serikali ya kuzizuia bado serikali imekuwa ikiwatoza kodi
wafanyabiashara hao kwa mizingo ya simu bandia wanazoziingiza nchini,”alisema
Juma.
Sikitu
Mwanakatwe, alisema tatizo la simu bandia litawaathiri watu wengi wakiwemo
wanasiasa, wasomi viongozi wa serikali na wakulima huko vijijini.
Alisema
kama wapo wanaonunua simu hizo bandia kwa kukusudia ni sawa lakini kuna wengine
wanauziwa baada ya kushawishiwa na wafanyabiashara kwamba ziko kwenye viwango
vya kimataifa.
Sikitu,
aliishauri mamlaka hiyo kuona kama kuna uwezekano na ikiwapendeza kuachana na
mpango huo hiku ikihakikisha kwa kushirikiana na Idara nyingine kuzuia
uingizaji wa simu hizo.
Meneja
Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi, alisema uzimaji wa simu hizo za bandia uko palepale, kwani zimegundulika kuwa zina madhara makubwa ya kiafya, kiuchumi na kwa ajili ya
kulinda usalama wa raia nchini na Taifa kwa ujumla.
“Unajua
simu hizo za bandia hivi sasa hazioani na mfumo wa mawasiliano wa taifa kwa
hiyo hata watumiaji wa simu hizo wanapozitumia kihalifu hawawezi kukamatwa kwa
hiyo ndiyo maana tunaziondoa sokoni.
“Kuna
watu wana masimu ya thamani wenyewe wakijua kuwa yako kwenye viwango kumbe hizo
ndiyo baadhi yake ziko kwenye simu bandia ni washauri kwamba wazihakiki huku wakitunza
stakabadhi zao siku zikizimwa wakadai fedha zao,waliowauzia wakikataa wakawashitaki kwa
vile kitendo walichofanya ni sawa na wizi,”alisema Mungi.
Mungi,
alisema mpango huo siyo wa Tanzania pekee bali imekuwa kushirikiana na baadhi
ya taasisi za kimataifa kama vile Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia
mawasiliano na shirika la afya duniani ambazi ndizo zilizokubaliana kusitisha
matumizi ya simu hizo bandia.
No comments:
Post a Comment