WAKAZI 65 ambao wamebomolewa nyumba zao katika bonde la
Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali ya Rais
John Magufuli, iwapatie msaada wa kibinadamu.
Wakazi hao wanahitaji msaada ikiwa ni pamoja na mahitaji
ya kijamii kwa vile tangu nyumba zao zilipobomolewa kimakosa ni zaidi ya miezi
sita huku wakiishi katika vibanda bila ya msaada wowote kutoka serikalini.
Wakizungumza na wandishi jijini jijini, kwa nyakati
tofauti, wakazi hao walisema wamekuwa wakiendelea kuishi katika mazingira
hayo magumu, kwa sababu ya kuasubiri uamuzi wa serikali ambayo iliahidi kwa
wale waliyokuwa wamejenga kutokana na vibali walivyopewa na maofisa wa serikali
wangefidiwa.
Miongoni mwa wakazi hao ni Sabrina Hilal (63), alisema
wamefikia hatua hiyo kwa vile wakati nyumba zao zinabomolewa wakazi hao
walikuwa na hati halali hivyo kuahidiwa kuwa wangelipwa fidia kwa ajili ya
kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine.
“Tunamuomba Rais Magufuli, atusaidie kwani tunadhani
yeye ndiyo mtu wa mwisho ambaye anaweza kutuokoa katika maisha haya magumu
kwenye hivi vibanda tunamoishi, atusaidie tuondoke hapa,” alisema Sabrina.
Alisema, tangu opeaheni ya bomoabomoa ya nyumba
zilizojengwa katika maeneo ya mabondeni na hatarishi ni zaidi ya miezi sita
sasa lakini walipopewa hadi kwamba wangefidiwa hakuna kitingozi yoyote wa
serikali aliyewatembelea kuja kujua hatima ya maisha ya wakazi hao.
“Sisi tumebomolewa nyumba zetu lakini tuna hati ambazo
tulipewa na Manspaa Kinondoni huku tukilipa hata kodi zaajengo, leo tunashangazwa
na ukimnya wa Manispaa yetu”alisema.
Alisema kuwa haki ya kuishi katika vibanda hivyo
kumekuwa na madhara makubwa sana ikiwemo watoto kubanwa na kifua kutokana na
hali ya hewa ya kipupwe.
Mwanaidi Idd, alisema kwa vile Rais Magufuli ameaikika
mara kwa mara nia ya serikali yake ni kusaidia wananchi hivyo anaamini kuwa
atalishugulikia suala hilo ili haki ipatikane.
Alisema wanamuomba Rais Magufuli, afanye ziara ya
kushtukiza ili kwenda kujionea maisha wanayoishi wananchi wake waliyompigia
kura katika uchaguzi mkuu uliyofanyika mwaka jana.
Aidha, Mwanaidi, alishauri serikali kuwachukulia hatua
za kishwria kwa maofisa wote wa manispaa ya Kinondoni, ambao walihusika katika
utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo hayo huku wakijua ni hatarishi.
No comments:
Post a Comment